Tunafanya nini na tunafanyaje?

kampuni ya Agreen Mind Limited inajishughulisha na kilimo cha parachichi, mbegu aina ya HASS pamoja na kusimamia miradi ya wakulima wengine kuanzia kwenye hatua ya kutafuta mashamba, kuandaa, kupanda, kutunza, kuvuna na kupeleka sokoni (Mnyororo wa thamani) na kutoa elimu ya ukombozi wa kifikra kuhusu uwekezaji na maisha bora. Pamoja na hayo, kampuni inatoa mpango wa kustaafu kwa wastaafu na wanaokaribia kustaafu.

Dhamira Yetu

Kuwekeza katika kilimo na kuzingatia matumizi bora ya rasilimali kwa malengo ya kuleta maisha bora kwa jamii inayotuzunguka.

Maono Yetu

Jamii endelevu yenye uchumi unaostawi.


Shughuli tunazofanya

  • Kilimo- Biashara
  • Elimu ya Ukombozi Wa Kifikra.
  • Viwanda na Masoko

SHUGHULI ZINAFANYIKA MKOANI IRINGA WILAYA YA KILOLO

Parachichi ni zao linalooteshwa katika ukanda wa baridi na katika ardhi yenye rutuba na maji ya kutosha. Iringa, Arusha, Mbeya, Morogoro, Njombe, Tanga na Kilimanjaro ni baadhi tu ya mikoa inayolima Parachichi kwa wingi hapa Tanzania. Kampuni ya Agreen Mind Limited. Tumechagua kulima Parachichi katika mkoa wa Iringa, Wilaya ya Kilolo.