Sisi ni Nani

Kampuni ya Agreen Mind Limited ni kampuni binafsi yenye ukomo kupitia Hisa. Kampuni hii imesajiliwa chini ya Sheria ya makampuni kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) nchini Tanzania, na kutunukiwa cheti cha usajili namba 152801440

Dhamira Yetu

Kuwekeza katika kilimo na kuzingatia matumizi bora ya rasilimali kwa malengo ya kuleta maisha bora kwa jamii inayotuzunguka.

Maono Yetu

Jamii endelevu yenye uchumi unaostawi.


Shughuli tunazofanya

  • Kilimo- Biashara
  • Elimu ya Ukombozi Wa Kifikra.
  • Viwanda na Masoko

SHUGHULI ZINAFANYIKA MKOANI IRINGA WILAYA YA KILOLO

Parachichi ni zao linalooteshwa katika ukanda wa baridi na katika ardhi yenye rotuba na maji ya kutosha. Iringa, Arusha, Mbeya, Morogoro, Njombe, Tanga na Kilimanjaro ni baadhi tu ya mikoa inayolima Parachichi kwa wingi hapa Tanzania. Kampuni ya Agreen Mind Limited tumechagua kulima Parachichi katika mkoa wa Iringa,Wilaya ya Kilolo.