SHUGHULI ZINAFANYIKA MKOANI IRINGA WILAYA YA KILOLO

Parachichi ni zao linalooteshwa katika ukanda wa baridi na katika ardhi yenye rotuba na maji ya kutosha. Iringa, Arusha, Mbeya, Morogoro, Njombe, Tanga na Kilimanjaro ni baadhi tu ya mikoa inayolima Parachichi kwa wingi hapa Tanzania. Kampuni ya Agreen Mind Limited tumechagua kulima Parachichi katika mkoa wa Iringa,Wilaya ya Kilolo.

SABABU ZA MSINGI KUCHAGUA IRINGA WILAYA YA KILOLO.

  • Hali ya hewa rafiki kwa zao la parachichi
  • Uwepo wa miundo mbinu ya barabara kuonekana ipo kwenye mchakato wa kuwekwa kwenye kiwango cha rami.
  • Uwepo wa mto Mtitu unaotililisha maji kwa mwaka mzima bila kukauka.
  • kuna ardhi kubwa yenye rotuba.